Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewatahadharisha wananchi Mkoani Kilimanjaro kuhifadhi chakula na kutokukitumia kwa ajili ya kutengenezea pombe za kienyeji kutokana na changamoto za ukame na ulioathiri msimu wa mavuno.
Chongolo ameyaema hayo hii leo Agosti 2, 2022 katika ziara yake ya siku tano Mkoani Kilimanjaro, kukagua uhai wa chama, kuhamasishwa sensa na kuangalia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia Ilani ya Cahama cha Mapinduzi.
Amesema, “Nchi mzima tunachangamoto ya mvua,kumekuwa na ukame,wito wangu kwenu kila mmoja ahifadhi chakula alichopata msimu huu,tutumie vizuri akiba hiyo,hifadhi chakula msipikie pombe au msiuze.”
Aidha Chongolo ameongeza kuwa, CCM itaisimamia Serikali ili kuhakikisha inawasaidia wananchi walioathirika na ukame, na kuwataka wafugaji kuuza sehemu ya mifugo yao kwa ajili kupata fedha za kununulia chakula na kuweka akiba mapema.