Akiendelea kushika Kasi ya Umaarufu kufuatia kufanya vibaya kwenye Masumbwi, Bondia Karim Mandonga ameibukia kwa Rais wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Injinia Hersi Said.

Mandonga ambeya alipoteza pambano lake dhidi ya Shaban Kaonekaka Jumamosi (Julai 30) mjini Songea mkoani Ruvuma, amekua maarufu kwa Watanzania kufuatia tambo zake kwenda kinyume na vitendo ulingoni.

Leo Mchana Bondia huyo kutoka Mkoani Morogoro alionekana katika picha ya pamoja na Rais wa Young African Injia Hersi Said akiwa amevalia Jezi nyeusi ya klabu hiyo.

Huenda kufika kwake ofisini kwa Rais wa Young Africans ikawa sehemu ya Shamra Shamra za kuelekea kilele cha Tamasha la Siku ya Wananchi, Jumamosi (Agosti 06), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Hata hivyo kiuhalisia inaeleza kuwa Mandonga ni shabiki mkubwa wa klabu ya Young Africans, hivyo kwa asilimia kubwa huenda akaonekana katika Tamasha hilo, ambalo huwakutanisha kwa pamoja Mashabiki, Wanachama, Wachezaji na Viongozi wa klabu hiyo Uwanja wa Benjamin Mkapa kila mwaka.

Halmashauri 100 zatikisa makusanyo ya mapato
Wananchi waaswa kutotumia mazao kutengenezea Pombe