Lydia Mollel – Morogoro.
Wananchi Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro, wameibua mjadala kufuatia baadhi yao kusemekana wameuza Ardhi waliyopewa na Serikali, kwa ajili ya shughuli za kilimo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuta takribani Mashambapori 60 Wilayani humo.
Mjadala huo, umeibuka katika kikao cha robo ya kwanza ya Mwaka cha Baraza la Madiwani mara baada ya Diwani wa kata ya Tindiga, Yahaya Mbaruku kuuliza swali kwa Mkurungenzi wa Halmashauti ya Wilaya ya Kilosa juu ya swala la ugawaji wa Mashamba hayo kwa Wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Kisena Mabuba amesema changamoto hiyo ya Wananchi kuuza maeneo waliyopewa ni jambo lililo kinyume na mpango wa serikali.
Mkuu wa Wilaya ya kilosa, Shaka Hamdu Shaka amesema asilimia 75 ya wananchi wa Kilosa maisha yao yanategemea Sekta ya kilimo, hivyo wameandaa utaratibu wa kuhakiki wale wote ambao wamepewa ardhi kujua ni wangapi wanatumia kama serikali ilivyoelekeza.