Lydia Mollel – Morogoro.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, imeomba Serikali kuongeza kasi kwa hatua zilizobaki katika utekelezaji wa ujenzi Reli ya kisasa SGR, ili iweze kuanza kufanya kazi.

Hayo yamejiri mara baada ya Kamati hiyo kutembelea vituo vya kupokea na kusambaza umeme Kingorwila na Msamvu Mkoani Morogoro, ili kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia za umeme kutoka Dar es salaam hadi Morogoro.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, David Mathayo David amesema wameridhishwa na hatua iliyofikiwa hadi sasa ya ujenzi huo, huku qkitoa rai kwa Wananchi kuchukua tahadhari katika maeneo ambayo ujenzi wa reli ya kisasa ya mwendokasi imepita, ili kuepukana na ajali zisizo za lazima.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amemtaka Mkandarasi anaesimamia Maboresho ya kituo cha kupooza umeme Msamvu kukamilisha ujenzi kwa wakati hadi kufikia Desemba 31, 2023 awe amekabidhi kwani tayari Serikali imeshakamilisha malipo ya ujenzi huo.

Hata hivyo, hadi sasa ujenzi wa njia za umeme katika ujenzi wa reli ya kisasa ya mwendokasi SGR umekamilika kwa asilimia 100 kutoka Dar es salam (kinyerezi ) hadi Morogoro na asilimia 99 kutoka Morogoro hadi Manyoni.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 12, 2023
Dkt. Biteko azindua kituo ujazaji Gesi asilia ya Magari