Bunge jipya la Kuwait litakuwa na wanaume pekee baada ya wanawake wote waliogombea kushindwa kwenye uchaguzi wa Jumamosi, hii ikiwa ni baada ya matokeo rasmi.
Takriban wagombea 326 katika taifa hilo la Ghuba, miongoni mwao wanawake 29 waligombea viti 50 vya bunge la kitaifa, katika wakati ambapo kunatolewa miito ya mageuzi na mabadiliko kwenye uchumi unaotegemea mafuta.
Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 2012, kwa bunge hilo kutokuwa na wanawake, hata hivyo mwanamke pekee aliyeingia katika bunge lililopita, alishinda katika uchaguzi wa marudio.
Mchambuzi wa siasa Mohammed al-Faili ameliambia shirika la habari la DPA kwamba raia wa Kuwait wanataka sauti zenye nguvu bungeni, ambazo wanawake hawana.