Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amewaagiza Wakurugenzi Watendaji wa Halamashauri zote kuhakikisha wanatenga maeneo mengi kwa ajili ya uanzishaji wa vituo ambavyo wananchi watakwenda kupata ushauri nasaha na kupima kwa hiari ikiwa ni sehemu ya kujikinga na Ukimwi.
Ametoa wito huo mjini Tabora wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya Ukimwi kwenye mkutano wa siku moja.
Amesema hatua hiyo ni muhimu kwa ajili ya kutoa elimu katika maeneo mengine yenye mkusanyiko wa watu wengi juu ya kujikinga kwa wale ambao bado hawajapata maambukizi na wale ambao tayari ili wapate dawa za kufubaza virusi(ARVs).
Aidha, Mwanri amesema kuwa utafiti umebaini kuna mwamko mdogo kwa wanaume kupima na kutumia dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARVs) na kutoa wito kwa wanaume kujenga tabia kuongozana na wake zao katika kwenda kupata ushauri nasaha na kupima VVU.
-
Video: JPM amkabidhi mwanafunzi milioni 3 za ujenzi wa vyoo shuleni kwao
-
Video: JPM atoa kauli kuhusu bomoabomoa Mang’ula
-
Video: Magufuli azindua daraja jipya lililopewa jina lake
“Baadhi ya wanaume wengi wanaogopa kwenda kupima mara nyingi wanasubiri majibu ya wake zao wakiona amepata majibu kuwa hana maambukizo naye anaamini kwamba yuko salama, jambo ambalo linaweza lisiwe kweli ni vema elimu itolewe ili wenza waende kupima wote,” amesema Mwanri.