Serikali Mpya ya Afghanistan imewataka wanawake wa taifa hilo wanaofanya kazi kubaki nyumbani hadi mifumo sahihi itakapowekwa kuhakikisha usalama wao.

Msemaji wa Serikali ya Talibani Zabihullah Mujahid, amezungumza na vyombo vya habari na kusema kuwa, maamuzi hayo yametoka na taratibu walizojiwekea hadi watakapojiridhisha wanawake wana usalama wa kutoka nje na kufanya shughuli zao za kijamii.

Maamuzi ya Serakali ya Taleban, yamekuja baada ya kuipindua Serikali iliyokua madarakani chini ya Rais Ashraf Ghani majuma mawili yaliyopita.


Hata hivyo Sheria mpya ya kuwataka wanawake kubaki nyumbani imepingwa vikali na Umoja wa Mataifa (UN) kwa kusema ni ukiukwaji wa haki za kibinaadamu

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Michelle Bachelet amesema kwamba haki za wanawake ni “Mstari mwekundu ambao Taliban hawafai kuvuka”.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari huko Kabul Jumanne, msemaji wa Taliban pia alizungumzia uokoaji unaoongozwa na Marekani kutoka mji mkuu, Kabul.

“Ni utaratibu wa muda mfupi,” msemaji Zabihullah Mujahid alisema, Taliban, ambao walitekeleza sheria kali za kiislamu wakati walipokuwa wakiongoza Afghanistan kabla ya 2001, walichukua udhibiti kamili wa nchi hiyo siku tisa zilizopita.

Uzi mpya Young Africans 2021/22
Mkurugenzi Tume ya TEHAMA azindua Tuzo