Kocha Msaidizi wa Geita Gold FC Mathias Wandiba amesema Simba SC haikuwa na Uwezo mkubwa sana dhidi ya kikosi chao katika mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jana Jumatano (Agosti 17), Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mabao ya Augustine Okrah, Moses Phiri na Clatous Chama yaliiwezesha Simba SC iliyokua nyumbani kuibuka na ushindi wa 3-0 mbele ya Mashabiki wachache waliojitokeza Uwanja wa Mkapa.

Wandiba amesema kwa asilimia 50 wachezaji wake walionyesha Uwezo mkubwa wa kuikabili Simba SC na kwa wenyeji wao nao walikua katika kiwango cha asilimia 50, hivyo kilichopatikana baada ya mchezo ni kama bahati kwao.

Amesema kiuhalisia anachokiona Simba SC walichowazidi ni Mazingira ya kuweka Kambi nchini Misri, lakini kwa upande wa Soka hakuna lolote ambalo lilikua geni kwao katika mchezo huo.

“Kimsingi Simba SC wametuzidi kwenye maandalizi ya msimu Lakini ndani ya uwanja tulikuwa 50 kwa 50 kwenye suala la kumiliki mpira, Ni MATOKEO tu ndio yameangukia upande wao kwakuwa walitumia nafasi” amesema Wandiba.

Ushindi huo wa 3-0 umeiwezesha Simba SC kukwea kileleni mwa Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kufuatia kuwa na idadi kubwa ya mabao, tofauti na timu nyingine zilizopata matokeo mazuri kwenye Mzunguuko wa kwanza ulianza rasmi Jumanne (Agosti 15).

Meena: Sheria ilikataliwa siku ya kwanza
Ajenda ya Usalama na Biashara zatawala mkutano SADC