Serikali nchini Gambia, imesema imezuia jaribio la mapinduzi ya kijeshi na kuwakamata wanajeshi wanne wanaoshukiwa kupanga njama ya kuupindua utawala wa kidemokrasia, wa Rais Adama Barrow.

Taarifa ya Jeshi la nchini humo, imeeleza bado inaendelea kuwasaka watu wengine watatu ambao nao wanatuhumiwa kuhusika na jaribio hilo la mapinduzi.

Rais wa Gambia, Adama Barrow. Picha ya GETTY IMAGE

Desemba 20, 2022 Shirika la Fedha Ulimwenguni IMF, liliidhinisha utoaji wa fedha kiasi cha dola milioni 27.41 kwa Gambia, ili kuliwezesha taifa la Afrika Magharibi, ili kukidhi mahitaji yake.

Hata hivyo, hakuna milio ya bunduki ambayo imeripotiwa kusikika, na hakuna dalili kwamba vikosi vya watiifu vimetumwa ili kulinda maeneo ya kimkakati.

Mecky Mexime: Sio matokeo mabaya kwetu
Aliou Cisse aingizwa kikaangoni Senegal