Waokoaji wa kuwatafuta manusura na majeruhi wa ajali ya tetemeko la ardhi Nchini Morocco, wamekuwa wakitumia mikono kutokana na ujosefu wa vifaa, huku mamlaka ikihangaika kufungua Barabara zilizojaa vifusi ili kufikisha vifaa.
Katika Vijiji vya mbali vya Milimani kusini mwa mji wa Marrakesh, waokoaji wanapambana kutafuta manusura baada ya kutokea kwa maafa hayo na Mataifa wahisani wakitangaza kupeleka misaada zaidi.
Hata hivyo, idadi rasmi ya vifo vilivyotangazwa mpaka sasa ni watu zaidi ya 2,100 lakini kumekuwa na tahadhari kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka, kutokana na ukubwa wa uharibifu unavyozidi kuongezeka.
Aidha, Wafanyakazi wa dharura kutoka nje ya Morocco nao wamejiunga na juhudi za uokoaji ili kutoa usaidizi unaohitajika kwani kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo unapunguza uwezekano wa kupata manusura.