Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amearifu kuwa wanajeshi wake wamewaua zaidi ya wanachama 560 wa kundi la waasi la DF linaloshirikiana na Islamic State, tangu walipoanzisha operesheni dhidi yao Desemba 2021.

Kundi linaloipinga Kampala la Allied Democratic Forces – ADF, linaendesha shughuli zake katika misitu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC, ambako linafanya mashambulizi ndani ya Congo na Uganda.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Baada ya kupata kibali toka DRC, Wanajeshi wa Uganda walianzisha operesheni dhidi ya ADF wakitaka kuharibu kambi zao na kuua au kuwakamata wapiganaji wa kundi hilo.

Tetemeko lauwa 300 Morocco
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 9, 2023