Vyombo vya usalama nchini Mali vimesema takribani Raia 49 na Wanajeshi 15 wameuawa, kufuatia shambulio la Wanamgambo wa Kiislamu wenye msimamo mkali kwenye kambi ya Jeshi.

Katika shambulio hilo, pia watu kadhaa walijeruhiwa, huku idadi ya waliofariki ikihofiwa huenda kuwa ikaongezeka.

Wanamgambo hao, mbali na kushambulia kituo cha Kijeshi, pia waliirushia sisasi boti iliyokuwa imebeba raia katika eneo  linalotenganisha miji ya Gao na Mopti.

Aidha, takriban Washambuliaji 50 waliuawa katika makabiliano hayo, na tayari Serikali ya mpito ya nchi hiyo imetangaza siku tatu za maombolezo ya Kitaifa.

Mali ni moja kati ya nchi kadhaa za Afrika Magharibi zinazokabiliana na uasi mkali wenye mafungamano na makundi ya al – Qaeda na Islamic State.

Taifa Stars yatoboa AFCON 2023
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 8, 2023