Bunge jipya la Katiba nchini Venezuela limepitisha sheria ya kuwashtaki viongozi wa upinzani kwa makosa ya uhaini na tuhuma za kuchochea nchi hiyo ikawekewa vikwazo vya kiuchumi na Marekani.
Bunge hilo limesema kuwa limekusudia kuwashughulikia viongozi wote wa upinzani nchini humo ambao wamesababisha nchi hiyo kuwekewa vikwazo na Marekani kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na matakwa ya wananchi wa kawaida wa Venezuela kwakuwa watakosa baadhi ya mahitaji yao msingi ambayo ni haki yao.
Aidha, Rais wa nchi hiyo, Nicolas Maduro mara kwa mara amekuwa akiwatuhumu viongozi wa upinzani kuwa upande wa Marekani, nchi ambayo amesema inajiandaa na kuivamia nchi hiyo Kijeshi.
-
Umoja wa Ulaya waunda mpango wa kukabiliana na wahamiaji haramu
-
Korea Kaskazini yaianzishia chokochoko Japan
-
Israel yaituhumu Iran, yaitaka iache mchezo mchafu
Hata hivyo, wiki iliyopita Rais wa Marekani, Donald Trump aliamuru kuiwekea vikwazo nchi hiyo na kuzuia mali zote za Rais Maduro kwa kile alichokiita kuwa nchi hiyo haifuati utawala wa kidemokrasia.