Uongozi wa Klabu ya Tabora United (Kitayosce) umedhamiria kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa kuwasajili wachezaji wawili wa Timu ya Taifa ya Burundi.

Timu hiyo iliyopanda daraja sambamba na JKT Tanzania imekaribia kunasa saini ya beki Derrick Mukombozi anayekipiga Nkana ya Zambia na kiungo ambaye jina lake halijafahamika kwa haraka, ambaye alikuwa akikinukisha wakati Burundi ikiifunga Namibia kwenye mechi za kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’.

Chanzo makini kutoka ndani ya Kitayosce kinasema Mukombozi alianza kufuatiliwa muda mrefu baada ya timu hiyo kupanda Ligi Kuu na katika mchezo wa juzi Uwanja wa Mkapa wakati Burundi ikiichapa 3-2 Namibia wachezaji hao walikuwa wakifuatiliwa na mabosi kwa karibu zaidi.

“Kilichokuwa kinasubiriwa ni kwasababu walikuwa kwenye majukumu yao ya timu ya taifa hivyo pande zote tayari zimekubaliana na kilichobaki watakuja nchini kumalizia taratibu nyingine.

Lazima timu iimarishwe kwani Ligi Kuu haitaki kwenda kwa kusuasua tunahitaji kuleta ushindani wa maana pale msimu utakapoanza basi tuwe tumejiandaa vizuri,” kimesema chanzo hicho.

Kimeongeza kuwa asilimia kubwa ya wachezaji waliokuwa wakicheza Ligi ya Championship wataachwa wakatafute maisha mengine na watakaobaki hawawezi kuzidi hata 10, huku akiweka bayana kwamba Kocha Fred Felix Minziro naye alikuwa anajadiliwa kupewa timu baada ya kuachana na Geita Gold.

Sauti imesikika, Waziri Mkuu kachukua hatua
Dereva, Mtengeneza Barabara chanzo cha ajali nchini