Katika kipindi hiki ambacho Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na wadau mbalimbali wakijikta katika kuendelea kusaidia wahanga wa maafa yaliyotokana na maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang huko mkoani Manyara, Wasanii nchini wameombwa kuungana kwa pamoja na kutoa michango yao kwa ajili ya kusaidia familia zilizo athirika na janga hilo.

Wito kwa wasanii kufanya hivyo umetolewa na Katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa BASATA’ Dkt. Kedmon Mapana wakati akizungumza na waandishi wa Habari leo Desemba 6, 2023 jijini Dar es salaam ambapo amesema ikiwa yupo msanii ambaye yuko tayari kwenda kutoa misaada, Baraza lipo tayari kumuunga mkono kwa kumsindikiza, aidha wasanii wanaweza kuwasilisha michango yao na Baraza hilo litawasilisha michango hiyo kwa niaba yao.

Dkt Mapana Ameongeza kuwa wakati nchi inapitia hiki kipindi cha maombolezo BASATA inafahamu kuwa Hanang kulikua na wasanii ambao wao na familia zao wameathirika hivyo linahimiza wasanii kuungana, kutoa pole na misaada mbali mbali kwa wahanga.

ALSO READY: BASATA YAVUNJA UKIMYA/ SAKATA LA NAY WA MITEGO/ DIAMOND ATAJWA / ONYO KALI/ ‘WAVUJISHA VIDEO CHAFU

Wachezaji Young Africans waahidi ushindi
Vijana wajadili njia za kuondoa umasikini, utegemezi