Mashabiki wa klabu ya Arsenal ni kama wamepoteza furaha baada ya kugundua jina la mwamuzi atakayechezesha mchezo wao wa kuamua hatima ya mbio zao za ubingwa wa kwenye Ligi Kuu England msimu huu dhidi ya Manchester City, Aprili 26.

Ni hivi, mwamuzi Michael Oliver ndiye atakayeshika filimbi katika mchezo huo na hili limewavuruga mashabiki wa Arsenal.

Mchezo huo utakayopigwa uwanjani Etihad, umebeba hatima ya ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu 2022/23.

Man City kwa sasa ipo nyuma kwa alama nne dhidi ya Arsenal, lakini wana mchezo mmoja mmoja huku sare mbili walizozopata katika michezo dhidi ya Liverpool na West Ham Utd zikiwarudisha katika ushindani mgumu.

Michael Oliver alikuwa mmoja waamuzi wa Kingereza waliochaguliwa kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 huko Qatar.

Wakati ikiwa hakuna kesi yoyote ya upendeleo kutoka kwa mwamuzi Oliver, lakini rekodi za mwamuzi huyo anapochezesha michezo ya Arsenal ndicho kitu kinachowatisha.

Arsenal imekumbana na vichapo mara 16 kwenye Ligi Kuu England katika mfululizo ikiwatibulia The Gunners katika mbio hizo na kuweka kwenye presha kubwa.

Ushindi kwa Man City katika mchezo huo utafuta matumaini ya Arsenal kuchukua ubingwa wa kwanza wa ligi baada ya kusubiri kwa miaka 19.

Kwa mujibu wa mechi hiyo, ndipo mechi ambazo zilichezeshwa na mwamuzi huyo, wakati upande wa pili wa Man City, wenyewe wameshinda mara 31, Oliver aliposhika filimbi.

Kingine ni kwamba tangu Oliver, 38, alipopandishwa kuchezesha Ligi Kuu England mwaka 2010, ndani ya muda huo, Man City imebeba mataji matano na hili wanalofukuzia ni la sita.

Hata hivyo, huo ni wasiwasi tu wa Arsenal, ambapo msimu huu wameshinda mechi zote nne zilizochezeshwa na Oliver.

Lakini, kingine kinachowavuruga ni mpango wa kumtaja mwamuzi David Coote kwenye VAR.

Thiago Silva amkosoa mmiliki wa Chelsea
Temeke: Wanne wa familia moja wafariki kwa kuvuta hewa chafu