Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda amesema Wizara itapima matokeo ya Watafiti wa ndani kulingana na kazi zao zinazo chapishwa katika majarida makubwa ulimwenguni.
Prof. Mkenda ameyasema hayo katika hafla ya kutangaza washindi wa Tuzo ya watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao, katika majarida yenye hadhi ya juu Kimataifa.
Jumla ya kiasi cha shilingi 1 Bilioni zilitengwa kwa ajili ya zoezi hilo, ikiwa ni hamasa kwa watafiti wa sayansi na Teknolojia nchini ambapo machapisho 82 yalipokelewa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, huku 71 kati ya hizo zilitoka katika vyuo vya elimu ya juu vya umma na 11 vyuo binafsi.
Sayansi ya Afya Shirikishi, Sayansi Asilia pamoja na Hisabati ndio nyanja Maalum zilizokuwa zimependekezwa kushindaniwa na hata hivyo wakati wa uhakiki wa machapisho 82 katika hatua sita pendekezwa na kamati iliyo chini ya wizara, ni machapisho 63 pekee ndiyo yaliyo kidhi vigezo.