Waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Thomas More Jimbo Kuu la Mbeya, wametakiwa kuzishinda dhamiri zao mbaya ili kutotenda matendo uhalifu katika jamii.

Hayo yalisemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi, Theopista Mallya, wakati aliposhiriki ibada ya misa takatifu na kutoa elimu kwa waumini walioshiriki ibada hiyo kuhusu madhara ya kutekeleza dhamiri mbaya ambayo inapelekea kufanya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto.

Kamanda Mallya alisema si jambo jema kwa muumini anayekuja kanisani kumcha Mumgu lakini anatekeleza dhamiri mbaya ambayo inampelekea kufanya ukatili na vitendo vya uhalifu.

“Kumcha Mungu ni kuyatenda yale yote aliyoyaelekeza katika biblia na vitabu vitakatifu pia kuyaishi ili kutokomeza vitendo viovu katika jamii na hapo tutakuwa tumeishinda dhamiri mbaya kwenye mioyo yetu,” alisema.

Wewe unaamini nini? Baki na imani yako,
Zaidi ya watu milioni kutoshiriki uchaguzi DRC