Ndege ya kampuni ya Edelweiss ya Uswisi aina ya Airbus 343 leo Oktoba 9, 2021 imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kilimanjaro KIA ikiwa na watalii 270 kutoka Uswisi.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari Maelezo Gerson Msigwa, ndege hiyo ya kampuni ya Eldeweiss itakuwa ikifanya safari za moja kwa moja kutoka Zurich – Uswisi hadi kilimanjaro Tanzania mara mbili kwa wiki.
Kuwasili kwa watalii hao ni hatua muhimu kwa nchi ya Tanzania katika kufungua milango zaidi ya kuongeza idadi ya watalii, na kuongeza idadi ya wafanyabiashara kuja nchini na wawekezaji pia.
Malengo ya serikali ya awamu ya sita chini ya rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha inafikia lengo la kuvutia watalii milioni tano ifikapo mwaka 2025.