Mbwa 438 na paka Tisa katika Halmashauri ya manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wamepatiwa chanjo ya kichaa Cha mbwa na dawa za minyoo, vitamin Ili kuwakinga wanyama hao na ugonjwa huo.

Aidha chanjo hiyo imetolewa bure kupitia ufadhili wa shirika la kutetea Haki na ustawi wa wanyama TAPO katika Viwanja vya magereza Kahama.

Akizungumza na Dar24news Dr Jerome Majaliwa Said kutoka katika hospitali ya wanyama Zonal Veterinary centre – Mwanza Amesema kuwa Kuna umuhimu mkubwa wa kuwapeleka mbwa na paka kupata chanjo hiyo Ili kumkimga mnyama asipate ugonjwa huo ambao anaweza akamuambukiza mwadamu .

Aidha Dr Jerome Amesema kuwa ni muhimu kutoa Elimu ya kutosha kwenye jamii Ili jamii iweze kutambua umuhimu wa chanjo hiyo ambayo huchanjwa mara Moja kwa mwaka lakini pia kujua athari za ugonjwa huo ambao ukimpata mwanadamu ni shida kuweza kupona.

Sambamba na hayo ametoa Rai kwa wananchi wote wanaofuga mbwa na paka watambue umuhimu wa kuchanja wanyama Ili kujiepusha na athari za ugonjwa wa kichaa Cha mbwa.

Watalii 270 wawasili nchini
Tanzania yavunja rekodi mauzo ya bidhaa nje ya nchi