Watu watano wamefariki, na wengine 20 kujeruhiwa katika shambulizi la Makombora ya Urusi katikati ya mji wa Kherson uliopo nchini Ukraine ambao ulikombolewa mikononi mwa vikosi vya Putin.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amelaani shambulio hilo na kulitaja kama uhalifu mwingine wa Urusi ikiwa ni siku muds mchache kabla ya sikukuu ya Krismasi na hivyo kuzua taharuki.
Naibu mkuu wa ofisi ya rais, Kyrylo Tymoshenko amechapisha picha za watu waliouwawa kwenye mtandao wake wa habari kupitia Telegraph ikiwa Nina mojawapo ya kuonesha tukio Hilo.
Aidha, Zelensky amesema picha hizo za wafu zinaweza kuripotiwa kwenye kwenye mitandao ya kijamii lakini maudhui nyeti bali ni maisha halisi ya raia wa Ukraine na kusema mji huo wa Kherson hivi karibuni ulikombolewa kutoka kwa uvamizi wa Urusi.