Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema amefuta sheria ya hukumu ya kifo na kubadili sheria ya ukosoaji wa kiongozi wa nchi kuwa kosa linaloadhibiwa kisheria. 

Msemaji wa rais, Anthony Bwalya amesema Hichilema ameidhinisha kanuni ya adhabu ya mwaka 2022 inayofuta adhabu ya kifo na kosa la kumkashifu rais, ambalo limekuwa kwenye  sheria vya Zambia kabla ya uhuru. 

Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema. Picha ya Daily Nation.

Hatua hiyo, imesifiwa na Wanaharakati wa haki nchini Zambia wakisema uamuzi wa kufuta sheria mbili za wakati wa ukoloni wa Uingereza ambazo haziendani na utawala wa kidemokrasia wa tiafa hilo ni sahihi.

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Sera ya Mazungumzo, Caroline Katotobwe amesema raia wa Zambia sasa watakuwa na uhuru wa kueleza maoni yao bila kuogopa kufunguliwa mashtaka.

Watano wafariki kwa shambulio la bomu
Mtoto wa miaka sita ajinyonga kwa Chandarua