Raia watano wa Iraqi wameuawa baada ya roketi kurushwa kwenye nyumba iliyokuwa karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad

Jeshi la Iraqi limesema Waathirika walikuwa wanawake wawili na watoto watatu kutoka kwa familia moja. Watoto wengine wawili walipata majeraa.

.

Mpaka kisasa hakuna kundi ambalo limedai kurusha roketi hiyo lakini uwanja wa ndege ikiwemo kambi ya jeshi ya Marekani, mara nyingi nyingi ndio inayolengwa na kulaumiwa pamoja wanamgambo wanaounga mkono Iran .

Hii ilikuwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi kadhaa raia wa kawaida kupata  kujeruhiwa.

Waziri Mkuu wa Iraqi Mustafa al-Kadhimi aliagiza kusimamishwa kazi kwa vikosi vya usalama katika uwanja wa ndege kufuatia kutokea kwa ajali hiyo  Na kusema kuwa maafisa watachukuliwa hatua kwa kushindwa kuchukua hatua na kuruhusu vitendo vya ukosefu wa usalama kama hivyo,

Kadhimi ametoa wito wa juhudi za pamoja”kumaliza uhalifu wa aina hiyo dhidi ya raia” na kuahidi kutoruhusu “magenge hayo kuwa huru wakati yanatatiza usalama bila ya kuadhibiwa”.

Kushindwa kwa Serikali ya Iraqi kusitisha mashambulizi ya roketi yanayorushwa kuelekezwa uwanja wa ndege na uwanja wa ubalozi wa Marekani huko Baghdad kumesababisha wasiwasi mkubwa.

Wiki iliyopita, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo inasemekana kwamba alimuonya rais Barham Salih kwa njia ya simu kwamba ubalozi huo utafungwa ikiwa mashambulizi hayo yataendelea.

Tangu mwezi Agosti, kumeshuhudiwa idadi ya mashambulizi sawa na hayo.

Mapema mwezi huu, Marekani ilitangaza kuwa itaondoa zaidi ya robo tatu ya jeshi lake nchini Iraq ndani ya wiki kadhaa.

Vigogo vyama vya siasa waitwa kwa msajili
Lema,Gambo wapigana vijembe