Ikiwa zimesalia siku 27 kufikia uchaguzi mkuu hapa nchini Wagombea nafasi ya ubunge jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ,na Mrisho Gambo wa Chama Cha Mapinduzi CCM ameonesha kutambiana kupitia kurasa za mitandao yao ya kijamii baada ya kutana na kupiga picha ya pamoja katika moja ya maeneo ya Jiji la Arusha .

 “Leo tumekutana Mbunge ninaeingia madarakani na Mbunge aliyemaliza muda wake! Ameniambia kuwa hajawahi kuwa na uchaguzi mgumu kama mwaka huu na amejiandaa kisaikolojia. CCM ni Chama kubwa hatuwezi kukosa kazi ya kumpa. Hakika nyumbani kumenoga” aliandika  Gambo .

Na kwa upande wake Godbless Lema ameandika yafuatayo

“Nimekutana na huyu kijana hapa Safari Bistro cafe, akaomba picha, nikasema ni sawa tu, kwani akose Ubunge hata na picha na mimi wajameni. Hali yake ni ya majonzi sana,” aliandika Lema

Hatua hii inamaanisha kuwa siasa si uadui bali ni ushindani wa hoja na kuna maisha baada ya uchaguzi .

Watano wauawa katika shambulio la roketi -Baghdad
Njia hii kutumika mapambano dhidi ya Malaria-Mara

Comments

comments