Mahakama ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma imewahukumu kifungo cha Miaka 30 Mussa Zuberi Amuri (28) na Saidi Shaibu Saidi (27) wote wakazi wa Kijiji cha Lukumbule Wilaya ya Tunduru baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia nguvu.

Akisoma hukumu hiyo ya kesi ya Jinai Na 59 ya mwaka 2023, Hakimu mkazi wa Mahakama, Kando alisema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasi na shaka, ambapo Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Februari 27, 2023 na kufikishwa mahakamani Machi 9, 2023 ambapo Novemba 2, 2023 hukumu ilitoka na wakapatikana na hatia ya kosa hilo.

Aidha, katika hukumu nyingine mkazi wa Kijiji cha Nyamizeze Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza, Samson Mibulo (35), naye amehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada kukiri kosa la kubaka baada ya kukumbwa na kesi hiyo ya jinai namba 122/2023, hukumu iliyotolewa Novemba 2, 2023 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Sengerema, Evod Kisoka.

Awali, akisoma maelezo ya kosa hilo mbele ya Hakimu Wakili wa Serikali, Morice Mtoi alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti mwezi Oktoba 2023 nyumbani kwake kijiji cha Nyamizeze na kukamatwaOktoba 23, 2023 na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa Wilaya ya Sengerema, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Tito Mohe baada ya kupata taarifa toka kwa wasamalia wema.

Wakili wa Serikali, Morice Mtoi alisema mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na Kifungu namba130(1) (2)(e) na 131(1) cha Sheria ya Kanuni ya adhabu sura ya 16 Toleo la mwaka 2022 ambapo licha ya maombi ya mshtakiwa (Mibulo), kuomba kupunguziwa adhabu, Mahakama imemhukumu kifungo hicho cha miaka 30, ili iwe fundisho kwa wengine.

Dilunga nje miezi mitatu
Gamondi atamba kuipasua Simba SC Jumapili