Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini TAKUKURU Mkoa wa Katavi inawachunguza watu 3, wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi kwa Makosa ya wizi wa dawa za Serikali.
Akitoa Taarifa kwa Waandishi wa Habari Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Christopher Nakua amebainisha watumishi hao ni ni Husseni Hassan Kimaro,Charles Daniel na Issack Muhigi ambao ni Wahudumu wa Afya Kituo cha Afya cha Ilembo.
Nakua ameeleza kuwa watuhumiwa hao watatu wanashikiliwa kwa kosa kuomba na kupokea Rushwa kwa wagonjwa waliokuwa wamelazwa Katika Kituo hicho.
TAKUKURU kuchunguza ubadhirifu wa fedha CAF
katika hatua nyingine Takukuru mkoani humo imerejesha Kiasi cha fedha shilingi Milioni 3 za Wakulima wa zao la Pamba Katika Wilaya ya Tanganyika.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Romuli Rojas John Ameishukuru Takukuru kwa kurejesha fedha hizo za wakulima wa Pamba Katika Halmashauri hiyo.
TAKUKURU yaokoa Sh. Bil. 12 mradi wa stendi Mbezi Luis
Aidha Naibu Katibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Faus TAKUKURU imerejesha Kiasi cha Shilingi Milioni 8 kutoka Kampuni ya Mamba Construction kama malipo ya Mafundi na Vibarua ambao kulikuwa na daili za kudhurumiwa