Wapiga mbizi watatu, raia wa Uingereza kati ya 15 waliohitimu mafunzo ya upigaji mbizi, ambao walikuwa wakisafiri na boti ya kusafirisha watalii iliyolipuka moto katika Bahari Nyekundu karibu na pwani ya Misri, wamefariki dunia.
Akithibitisha vifo hivyo, Msemaji wa Scuba Travel amsema wageni wake waliangamia wakati mashua ya ukubwa wa wastani ya kupiga mbizi, iitwayo Hurricane, ilipowaka moto karibu na mji wa mapumziko wa Marsa Alam hapo jana Juni 11, 2023.
Amesema, “kwa masikitiko makubwa kwamba sisi, kama waendeshaji watalii, kwa mioyo mizito, lazima tukubali kwamba wageni wetu watatu waliothaminiwa sana wa kupiga mbizi, waliangamia katika tukio hilo la kusikitisha.”
Taarifa hiyo iliongeza: “Wakati moto ulipozuka, wapiga mbizi 12 walikuwa wakishiriki katika mkutano mfupi kwenye bodi, wakati waliopotea waliamua kutopiga mbizi asubuhi hiyo”, na hapo awali mamlaka nchini Misri ilisema uchunguzi wa awali unaonesha saketi fupi ya umeme kwenye chumba cha injini ya boti ilipiga shoti.