Wizara ya Elimu nchini Niger, imesema zaidi ya shule 900 zimefungwa kutokana na ukosefu wa usalama huko Tillabéri kusini-magharibi mwa taifa hilo eneo ambalo linalengwa mara kwa mara na mashambulizi ya wanajihadi.

Wizara hiyo imesema, inasema inajitahidi kutafuta suluhu ya tatizo hilo ili kuhakikish akuwa utoaji wa elimu unaendelea kwa kuimarisha ulinzi wa eneo hili na maeneo mengine huku Walimu wakisema ili huduma iendelee wanahitaji usalama wao.

Waziri wa Elimu wa Niger, Ibrahim Natatou amesema asilimia 18 ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hawaendi tena shule huko Tillabéri, sawa na takriban wanafunzi 79,000, kati ya 438,000 waliopo katika shule mbalimbali za eneo hilo.

Amesema, “hii ni asilimia kubwa sana, vituo zinazowakusanya wanafunzi, migahawa ya dharura kwa wanafunzi kwa mfano Shule inapofungwa, baadhi ya wanafunzi huenda shule nyingine, lakini wengine huacha shule kwa kukimbia wakiogopa kutekwa au kuuawa.”

Lautaro Martinez gumzo usajili Ulaya
Bodi Simba SC yapokea ripoti ya Robertinho