Wenyeviti wa Kamati za Fedha na Uchumi, Wakurugenzi watendaji wa Wilaya, Wakuu wa Idara, Kamati za Zabuni na Vitengo vya ununuzi na Ugavi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Kilimanjaro wanatarajia kupata mafunzo ya siku tano yanayolenga kutatua changamoto za utekelezaji wa sheria za ununuzi wa umma na kanuni zake.

Mafunzo hayo yanatolewa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) ambapo mafunzo hayo yameanza Mei 8, na yanatarajiwa kumalizika Mei 12, mwaka huu mkoani Kilimanjaro.

Aidha, Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi imeamua kugharamia utoaji wa mafunzo hayo kama sehemu ya utekelezaji wajibu wake kwa jamii “Corporate Social Responsibility”  kwa mwaka wa fedha 2016/18 ambapo Bodi itawajengea uwezo wa kutekeleza majukumu kwenye eneo la ununuzi na ugavi.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Mahusiano ya Umma imesema kuwa lengo kubwa ni kutatua changamoto zinazotokana na mapungufu yaliyoainishwa na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).

 

Picha: Majaliwa afungua mafunzo ya wakuu wa wilaya, wakurugenzi
Video: Serikali kuwalipa fidia wakazi wa kipunguni