Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani amesema kuwa Serikali kupitia Wizara hiyo imetenga Shilingi bilioni thelathini(30) katika mwaka wa fedha 2017/2018 ili kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi wa Kipunguni wanaopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege.

Ameyasema hayo mapema hii leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa.

Amesema kuwa Serikali imechelewa kuwalipa fidia wananchi hao kutokana na uhaba wa fedha, huku akisema kwa sasa Serikali imeanza kuwalipa fidia kwa awamu ambapo mwaka 2009/10 wakazi 1500 wa eneo la Kipawa walilipwa shilingi bilioni 18 ambapo zoezi hilo lilikamilika januari 2010.

“Ni kweli Serikali ilifanya uthamini wa mali za wananchi ili kupisha upanuzi wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Dar es Salaam mwishoni wa miaka ya 90 ambapo maeneo yaliyoainishwa kwa ajili ya upanuzi huo ni Kipawa,Kigilagila na Kipunguni”,Amesema Ngonyani.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Mwaka 2009/10 wakazi wapatao 1500 wa eneo la Kipawa walilipwa fidia  zinazofikia shilingi bilioni 18 ambapo zoezi hilo lilikamilika Januari 2010.

 

Watendaji na wataalamu wa manunuzi kupigwa msasa
Prof. Muhongo aahidi neema kwa wachimbaji wadogo wadogo wa madini