Takriban watoto wapatao 300,000 wanazaliwa na tatizo la Seli Mundu duniani kote ambapo kwa Tanzania kila mwaka huzaliwa watoto 11,000 huku watoto 6,000 kati yao wakifikiwa na huduma za kliniki.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa huduma za kibingwa za upandikizaji wa uloto (Bone Marrow Transplant) hasa kwa watu wenye Seli Mundu (Sickle Cell).

“Watoto wanaozaliwa na tatizo la seli mundu huwa wanapata maumivu ya mara kwa mara ya viungo, wanakuwa na tatizo la kupungukiwa damu, wanakosa masomo kwa miezi mingi,” amesema.

Aidha, ameongeza kuwa “kuna mzazi amesema mwanaye alikuwa anahudhuria masomo kwa miezi mitatu tu kati ya 10 anayopaswa kuwepo shuleni, kutokana na tatizo hili la seli mundu,” amesema.

CAF Super League yaishurutisha Simba SC kusajili
Yahya Mbegu kumsaidia Tshabalala Simba SC