Serikali nchini Jamuhuri ya kidemocrasia ya Kongo imethibitisha kuwakamata na kuwaweka chini ya ulinzi washukiwa 11 kwa mauaji ya Daktari wiki iliyopita ambaye alikuwa anafanya kazi chini ya shirika la Afya duniani WHO kupambana na mlipuko wa ugojwa wa Ebora nchini humo.
Jaji wa mahakama ya kijeshi katiaka kanda ya Mashariki ya kivu, Colonel Kumbu Ngoma, ameeleza kuwa kati ya watuhumiwa waliokamatwa watatu ndiyo wanahisiwa kuwa walifyatua risasi April 19 na kusababisha mauaji ya daktari Richard Valery Mouzoko na wengine wanne wamekamatwa kwa kosa la kushirikiana na wauaji.
“Tuna matumaini kuwa hawa washukiwa waliokamatwa, vyombo vya usalama vitaweza kuwabaini wauaji sahihi na kupelekea haki kutendeka kwa yeyote aliyehusika na mauaji ya daktari” waziri wa afya wa DRC ameeleza hayo katika taarifa yake.
Dr. Mouzoko alipigwa risasi na kufariki katika eneo la mashariki ya Butembo, na shika la afya WHO limesema kuwa alikuwa na moja kati ya madaktari wanaosaidia kutibu wagonjwa wa Ebola DRC tokea mwezi wa nane 2018 Kaskazini mwa Kivu.
Mlipoko wa ugonjwa wa ebola DRC umeingia katika rekodi mbaya kwa kuua watu wengi zaidi baada ya ule uliotokea Afrika Magharibi 20014-2016, ulioua watu zaidi ya 11, 300, ambapo hadi sasa watu zaidi ya 885 wamefariki DRC.