Watu 12 ikiwa ni pamoja na polisi mmoja wameuawa baada ya mtu mwenye bunduki kuingia katika baa jijini Califonia nchini Marekani na kuanza kufyatua risasi.
Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Ventura, Geoff Dean amesema kuwa mshambuliaji huyo pia ameuawa ingawa haikufahamika mara moja aliuawa na nani.
Watu wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulizi hilo ambalo limetokea katika kitongoji cha Thousand Oaks nje kidogo ya mji wa Los Angeles. ambapo miongoni mwa waliouawa ni pamoja na polisi wa siku nyingi aliyekuwa kazini kwa miaka 29, Sajenti Ron Helus.
“Sajenti helus amekufa baada ya kufikishwa hospitali. nasema tu inaweza kuwa ugaidi kwa sababu huko ndiko tunakoenda siku hizi likitokea tukio kama hili. hakuna sababu yoyote tunayoifahamu mpaka sasa katika mauaji haya mabaya. Sina lolote linalofanya nidhanie hivyo, au FBI, kwamba ni ugaidi, lakini bila shaka tunaangalia hilo pia,”amesema mkuu wa Polisi Geoff Dean
Aidha, maelezo kuhusu shambulizi hilo yamekuwa yakitofautiana huku ripoti za awali zikisema mshambuliaji amekamatwa na wengine kusema ameuawa.
-
Ikulu ya Marekani yafuta kibali cha mwandishi aliyejibizana na Trump
-
Prince wa Saudi Arabia adai mwandishi aliyeuawa alikuwa hatari
-
Mwanasheria mkuu wa Marekani ajiuzulu
Hata hivyo, baadhi ya mashahidi waliliambia shirika la utangazaji la CNN kuwa baa hiyo ilikuwa imejaa vijana wengi wa vyuo vikuu kwa ajili ya kunywa na kucheza dansi.