Serikali ya Korea Kusini imeripoti kuwa takriban watu 91 waliopona virusi vya Corona wamepata tena maambukizi kwa mara ya pili.
Mkurugenzi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa nchini humo, Jeong Eun-kyeong amesema kuna uwezekano mkubwa virusi hivyo vilikuwa vimelala (dormant) na sio kwamba watu hao wameambukizwa upya.
Wataalamu wanasema huenda vipimo walivyofanyiwa watu hao vilionesha majibu ya uongo au baadhi ya virusi vilibaki mwilini ila havikuwa na madhara.
undani wa jambo hilo unaendelea kuchunguzwa kwani wataalamu wa afya wa Korea Kusini bado hawajafahamu kinachosababisha hali hiyo iliyozua taharuki.
Imelezwa kuwa hali ya wagonjwa wa covid 19kupata maambukizi baada ya kupona ni suala ambalo linahofiwa kimataifa kwakuwa nchi nyingi zinatamani walioathirika watakuwa na kinga ya mwili ya kutosha itakayowazuia kuambukizwa tena.