Virusi vya corona vinaweza kumuathiri yeyote, lakini watu wenye matatizo ya kiafya, wazee wale ambao mfumo wao wa kinga ya mwili umedhoofika na watu wenye magonjwa ya kudumu ukiwemo moyo, kisukari, au pumu wana hatari zaidi ya kuathiriwa, halikadharika wavutaji wa sigara.

Mkurugenzi mkuu wa misaada ya kiafya nchini Uingereza, Ash,Deborah Arnott, amethibitisha hilo na kutoa ushauri kwa wanaovuta sana sigara wanapaswa kupunguza au kujaribu kuacha kabisa uvutaji ili kupunguza hatari iwapo watapatwa na virusi vya corona.

“Wavutaji wa sigara wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya mfumo wa kupumua na wana uwezekano mkubwa mara mbili wa kupata maradhi ya mapafu- pneumonia kuliko wasiovuta sigara ,” amesema Arnott.

Watu wengi huanza kupona haraka ugonjwa wa virusi vya corona baada ya kupumzika kwa siku kadhaa. Kwa baadhi ya watu , inaweza kuwasababishia kuugua sana na wengine hata kufariki.

Imeelezwa kuwa dalili za Cororna ni sawa na za magonjwa mengine ambayo ni ya kawaida, kama vile mafua na homa, joto la juu ya mwili na kushindwa kupumua.

Janga la Ebola bado laitafuna Congo, mmoja afariki dunia
watu 91 waliopona Corona Korea kusini wamepata tena