Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limewashikilia watu 47 wanaotuhumiwa kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya, huku likifanikiwa kukamata misokoto 269, miche 13 ya bangi na kilogramu 32,9 za mitungi.
Matukio hayo yametokea katika msako mkali uliofanywa na kikosi maalumu cha jeshi hilo ndani ya siku nne katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Kilimanjaro.
Akitoa taarifa hiyo Kamishna wa Jeshi la OPolisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Mwandamizi Msaidizi Wilbroad Mutafungwa ametaja majina ya watuhumiwa hao na kueleza kuwa watuhumiwa hao tayari wamekematwa na wapo katika hatua mbali mbali za kiupelelezi na taratibu zikikamilika watafikishwa mahakamani.
Kati ya watuhumiwa hao 47, wapo watoto wawili wa miaka 17, wanawake 15, na wanaume 32 akiwemo mzee mwenye umri wa miaka 60.