Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameshangazwa na baadhi ya taarifa ambazo zilisambazwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii zakutaka kumgombanisha yeye na baadhi ya viongozi wenzake wa Serikali.

Waziri Nape kupitia ukurasa wake wa Tweeter ameandika kuwa amesikitishwa sana na si sawa , kwani watu wanachukua na kutafsiri watakavyo kwa faida zao

Kupitia ukurasa wake huo, Waziri Nape alinukuliwa kwa kaundika kuwa ”Ujinga ni mzigo mkubwa sana!! Omba busara ya Mungu kwa kila jambo kuliko utajiri na kiburi!”

Waziri Nape katika ‘tweet’ yake aliambatanisha na kipande cha video cha Mchungaji Christopher Mwakasege akisema ”Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu, sio kwamba hana akili bali amepungukiwa”.

Waziri Nape amesema alichokiandika hakijamlenga na wala hajakiweka kwa makusudi yoyote yenye nia ya kumsema kiongozi yeyote, ni utaratibu wake kusoma masomo ya Mwakasege.

 

 

 

Watuhumiwa 47 dawa za kulevya wadakwa
AC Milan Wapanga Mipango Kwa Sanchez, Lukaku