Watumiaji wa Dawa za kulevya wamekuwa wakihisi, kuona au kusikia vitu visivyokuwepo tofauti na uhalisia na kwamba huhisi raha isiyo kifani au furaha ambayo haifananishi na kitu chochote na kwamba utumiaji wa dawa hizo husababisha matatizo mbalimbali ikiwemo changamoto ya Afya ya Akili.
Hayo yamebainishwa hii leo Novemba 13, 2023 jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya – DCEA, Dkt. Paul Mfisi ambaye ameongeza kuwa uraibu wa Dawa za kulevya Heather utendaji kazi wa Ubongo.
Amesema, Bangi ni mmea haramu unaoongoza kwa kupatīkana na kutumiwa n watu wengi Nchini, ikifuatiwa na Heroin, Mirungi na Cocaine ambayo watumiaji huwa na sababu mbalimbali ikiwemo kuzuia kulala wakati wa safari hasa kwa Madereva na watendaji wa kazi ngumu.
“Zamani Babu zetu walitumia Bangi kwa kupata furaha au kulala, matambiko au sherehe za jadi na haikuwadhuru kama sasa kwani walikuwa wakitumia kwa sababu maalum lakini haikuwa na madhara makubwa kama ilivto sasa,” amesema Dkt. Mfisi.
Hata hivyo, amesema jamii inapaswa kushirikiana na mamlaka ili kufanikisha mapambano ya Dawa za kulevya kwani Vijana wengi wanaotumia hussein muda mfupi na kwamba hupunguza nguvu kazi ya Taifa na huathirika kiafya na huleta matatizo ya ubongo.