Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali inaandaa sheria maalumu ya mtu kuwa na laini moja ya simu kutoka kampuni lengo likiwa ni kudhibiti wahalifu mtandaoni
Amesema hayo katika mkutano wa watendaji wakuu wa kampuni za simu kujadili mambo muhimu wakati wa kuelekea awamu ya sita ya mradi wa mawasiliano maeneo ya mipakani na kanda maalumu.
“Nadhani kampuni zingine, lakini sio zote zina watu ambao sio wa kweli na wanafanya kazi na wahalifu kwa kutoa habari za siri za wateja kwa nia ovu. Hatutavumilia kuchukua hatua dhidi ya kampuni yoyote itakayotuhumiwa kuvujisha habari za wateja,” amesema Dkt. Ndugulile.
Dkt. Ndugulile amesema ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuangalia jinsi ya kutumia mfumo wa kuaminika zaidi kwa wateja kuthibitisha namba zao na kwa wale ambao hawawatambui, wanapaswa kufutiwa au kuzimwa kutoka katika mfumo.
“Hakuna haja ya kukaa na namba za watu kwa mfano mtu amesajili laini nyingi na ninyi TCRA mna nguvu na mifumo ya kutambua nani ana laini nyingi, wacha tufanye hivyo na tumalize kesi hizi,”
Naye, Mkurugenzi wa ufundi kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Andrew Lupembe amesema wapo tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha huduma ya mawasiliano inafikia malengo.
Naye, Mwakilishi wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Dk prosper Mafole alisema wapo tayari kushirikiana na Serikali kuboresha huduma ya mawasiliano nchini.