Mtandao wa kijamii wa Twitter umetangaza jaribio lake la kuongeza idadi ya maneno ya ujumbe ambayo mtu anaweza kuandika kwenye mtandao huo.
Kampuni ya Twitter imetoa taarifa kuwa idadi ya maneno ya ujumbe ambayo mtu anaweza kuandika kwa mara moja itaongezeka hadi kufikia 280 ambayo ni mara mbili ya kiwango cha idadi ya maneno yaliyopo kwa sasa.
Mtandao huu ambao umekuwa na idadi ya zaidi watumiaji milioni mia tatu,umekuwa ukikabiliwa na changamoto ya ukuaji na hivyo inatafuta namna mbalimbali za kukuza wigo wa watumiaji.
-
Mtandao wa WhatsApp wafutwa China
-
Video: DataVision kugeuza simu za wanafunzi kuwa kompyuta za kujifunzia
-
Muanzilishi Wa Facebook Aula Kielimu Chuo Kikuu Cha Harvard
Litahusishwa kundi dogo la watumiaji wa mtandao huo katika mchakato wa jaribio hilo la kuongeza idadi ya maneno ya kuandika.
Kampuni hiyo imesema hiyo ni hatua ya kutatua moja ya changamoto ambayo imekuwa ikiwasumbua watumiaji wengi.