Maofisa 8 wa taasisi tatu tofauti, ikiwemo TRA, TBS na idara ya mifugo katika kituo cha forodha kilichopo mpaka wa Horohoro wamesimamishwa kazi kwa madai ya kukosa maadili katika eneo la kazi.
Hatua hiyo imechukuliwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella ambae amesema kumekuwa na malalamiko ya baadhi ya wafanyabiashara kuwa vitendo vya rushwa vimekithiri katika ofisi za watumishi wa serikali katika boda hiyo.
Shigella ameeleza kuwa aliamua kuunda kamati maalumu ya uchunguzi iliyoanza kazi yake Novemba 18 kwajili ya kuchunguza mwenendo wa watumishi hao.
“Hapa wamegeuza kuwa ni shamba la bibi, hawa wanaenda kwenye taratibu za kiuchunguzi na vyombo vya dola viwachukue wakaanze kutoa maelezo kwanini wasipelekwe mahakamani,” amesema Shigelle.
aidha amesema kuwa endapo watabainika kuvunja maadili ya kazi serikali itawaleta watumishi wengine.