Johansen Buberwa – Kagera.
Watumishi wa Serikali wametakiwa kuwa na lugha nzuri na kuacha dharau kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi – CCM, pamoja na Wananchi wanaowatumikia, badala yake warudi kwenye maadili ya utumishi wao.
Kauli hiyo, imetolewa Mkoani Kagera na Mjumbe wa Halmashari kuu ya Taifa MNEC, Livingston Lusinde wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 47 ya CCM yaliyofanyika uwanja wa Fatma.
Lusinde, alimuwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ni mlezi wa chama hicho Kanda ya Ziwa na kusema CCM ndicho chama kilichowapatia ridhaa ya kuwatumikia Wananchi hivyo waache kuwadharau.