Watumishi wa Umma wameonywa kuhusu matumizi mabaya ya taarifa za serikali za siri na za kawaida kuzitoa kwa watu ambao sio walengwa wa taarifa hizo ambazo ni nyeti na ni siri ya Serikali.
Onyo hilo limetolewa hii leo Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Maadili kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Lambert Chialo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya Usalama wa Taifa Na. 3 ya mwaka 1970 na marekebisho yake, Ibara ya 5(a) na (b), adhabu ya uvujaji wa siri ni kifungo kisichozidi miaka 20.
“Hivi karibuni tumeshuhudia taarifa za serikali za siri zikitumwa katika vyombo vya habari pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii kitu ambacho ni kosa kisheria na ni kinyume cha Kanuni za Maadili ambapo inasisitizwa kuwa na matumizi sahihi ya taarifa,”amesema Chialo.
Amesema kuwa lengo la serikali si kuficha taarifa kwa wadau wake, bali taarifa zinazotolewa zinapaswa kutolewa kwa utaratibu maalumu na kupelekwa kwa watu wanaopaswa kupokea taarifa hizo.
-
Serikali kuanzisha Fao la Upotevu wa Ajira
-
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Septemba 12, 2017
-
Video: Makonda azidi kuiboresha Dar, biashara ya magari kufanyika Kigamboni tu
Hata hivyo, ameongeza kuwa baadhi ya watumishi wamekuwa wakitumia nafasi walizonazo kwa manufaa yao binafsi na sio ya Umma, kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na watumishi watakaogundulika watawajibishwa kwa mujibu wa Kanuni na taratibu.