Watumishi wanaotarajia kustaafu wameaswa kuzingatia mabadiliko ya maisha kutoka katika utumishi wa umma kwenda katika mfumo wa maisha ya kawaida na kujiepusha kufanya miradi ambayo hawana ujuzi nayo.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Doroth Mwaluko ambapo amesema kuwa Ofisi hiyo inatambua umuhimu wa wastaafu na faida za kujiandaa kustaafu.
Amesema kuwa kila mtumishi wa umma lazima atambue kuwa ni mstaafu mtarajiwa hivyo kujiandaa kwake ni jambo muhimu
“ Kuna umuhimu mkubwa wa kutambua kuwa suala la kustaafu ni la kila mmoa wetu na ni muhimu kujiandaa vyema na maisha mapya ambayo kimsingi yatakuwa tofauti na haya ya utumishi wa umma mliyo nayo kwa sasa,”amesema Mwaluko
Kwa upande wake Muwezeshaji Kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni Jijini Dar es Salaam, Peter Seme amesema kuwa watumishi hao wanaotarajia kustaafu watajifunza mambo mengi yakuwawezesha kuendelea na maisha yao kama kawaida hata baada ya kustaafu.
Naye mmoja wa watumishi hao, Esamo Sawaki amesema kuwa wanaipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuandaa mafunzo hayo kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi hiyo ili waweze kukabiliana na changamaoto zinazoweza kujitokeza baada ya kustaafu.
-
Watumishi waaswa kuzingatia mabadiliko ya maisha baada ya kustaafu
-
Tanzania kinara wa Amani nchi za Afrika Mashariki
-
Makonda atimiza ahadi yake kwa klabu ya Yanga
Mafunzo yakuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu hivi karibuni yanafanyika Jijini Dodoma kwa siku tano yakiwashirikisha watumishi hao kutoka kada mbalimbali.