Mkuu wa kitengo cha Kilimo Biashara wa NMB Makao Makuu, Nsolo Mlozi amesema wamefanya mabadiliko makubwa kwa kuanza kutoa uwezeshaji kwa kundi la Wakulima, Wavuvi na Wafugaji kwa kuwakopesha zana za Uvuvi, Kilimo na ufugaji wakilenga kuwainua kiuchumi makundi hayo nchini.
Mlozi ameyasema hayo hivi karibuni na kuongeza kuwa, Sekta ya Kibenki ni muhimu katika uimarishaji wa maendeleo ya nchi yoyote duniani, hivyo wameamua kutoa mikopo hiyo kwa Wavuvi, Wakulima na Wafugaji nchini kama sehemu moja wapo ya ukuzaji wa pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kiujumla.
Awali akizungumzia mkakati wa Serikali kuhakikisha Wilaya ya Mafia inafikika kiurahisi na Wananchi na Watalii Mkuu wa Wilaya ya Mafia Zephania Sumaye amesema serikali imetenga zaidi ya shilingi billioni kwaajili ya kuleta kivuko kikubwa kipya ikiwa ni pamoja na kuelea na uboreshaji wa uwanja wa ndege Wilaya ya mafia.
Meneja wa Kanda ya Mashariki kusini, Lilian amewataadharisha uongozi wa Wilaya Mafia mkoani katika uwekezaji huo mkubwa wa Sekta ya utalii kwa kuhakikisha wanahimalisha utunzaji wa mazingira, ili kuwa na matokeo ya uchumi wa Buluu endelevu.