Johansen Buberwa – Kagera.

Serikali imewatoa hofu wawekezaji waliowekeza nchini na wanaotaka kuja kuwekeza kwenye zao la Kahawa kuwa tayari Wizara ya Viwanda na Biashara imeaza kulishugulikia tatizo la ushindani la upatikanaji wa malighafi na bei nzuri kwa Wakulima na Viwanda.

Kauli hiyo, imetoleea na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji katika ziara yake ya siku moja Mkoani Kagera, alipotembelea kiwanda cha Amimza cha Bukoba na kusema uwepo wa Malighafi imekuwa ni fursa kwa Wawekezaji na uhakika wa Soko umefanya wanunuzi kuwa wengi.

Amesema, hali hiyo ni furusa kwa wakulima kwani awali ilikuwepo changamoto ndani ya kipindi cha miaka miwili na sasa bei ni shilingi 900 kwa kilo moja na huenda hadi shilingi 3,000 kwa kilo.

Kwa upande wake mwekezaji wa kiwanda ya Amimza, Amry Hamza amesema kwasasa wana uwezo wa kuzalisha Kahawa ya unga tani elfu sita ambazo ni sawa na tani elfu 15 hadi 18 ya kahawa safi.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Toba Nguvila amesema watahakikisha Kahawa ghafi haivushwi kwenda nje ya nchi na kupitia Wilaya zote watahakikisha viwanda havikosi malighafi na vinalindwa, ili kuhakikisha vinamudu ushindani uliopo pamoja na kuboresha uzalishaji  ili uchumi wa Kagera ukue na tayari mpaka sasa miche Milioni 20 kupitia Wizara ya Kilimo imesambazwa kwa wakulima katika kipindi cha Mvua.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Wakili Stephano Byabato ambaye pia ni Naibu waziri wa Mambo ya Nje ameshukuru Waziri Kijaji kwa kutmembelea mwekezaji ndani ya Jimbo lake na kusema kiwanda hicho ni muhimu sana kwa uchumi wa Kagera kwani uwezo wa kuzalisha na kutoa Ajira kwa Wananchi 400 wenye mkataba wa kudumu na wengine1500 wana mkataba wa muda.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 25, 2023
Mwendokasi, kuzidisha abiria chanzo ajali msimu wa sikukuu