Wazee wametakiwa kurudisha utamaduni wa kuongea na Vijana wao na kuwarudisha katika mstari ili kuenzi mila na tamaduni chanya zilizokuwepo tangu enzi za zamani.

Hayo yamesemwa na Polisi Kata wa Kata ya Mtimbira Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Henry Mwangake alipokutana na Wazee katika eneo la standi ya Mtimbira.

Amesema, “Wazee wa siku hizi wamekuwa wazito kuzungumza na vijana wao hata wanapowaona wanapotoka kimaadili jambo ambalo kimepelekea mmomonyoko wa Maadili katika jamii hali ambayo inachangia kutokea kwa vitendo vya uhalifu kwenye Jamii.”

Aidha, alitumia fursa hiyo kuongea na Wafanyabiashara wa fedha (Mawakala) juu ya namna ya kuwatambua matapeli na kujiepusha nao bila kusahau kutoa taarifa kwa haraka ili wachukuliwe hatua.

Mo Salah: Ninamtamani Kevin De Bruyne
Ugomvi wa uke wenza wasababisha uharibifu wa mali