Shirika la Afya Duniani (WHO), limetangaza kuzindua kampeni ya kuzuia matukio ya kujitoa mhanga Barani Afrika, eneo ambalo linatajwa kuwa na kiwango kikubwa zaidi cha vifo vya kujitoa mhanga Duniani.

Ofisi ya WHO ya kanda ya Afrika inasema, “Takriban watu 11 kwa kila 100,000 hufa katika kanda ya Afrika, ambayo ni ya juu kuliko wastani wa kimataifa wa visa tisa vya kujiua kwa kila watu 100,000.”

Aidha, imebanisha kuwa, “Afŕika ni nyumbani kwa nchi sita kati ya kumi zenye viwango vya juu zaidi vya kujiua dunianina mbinu zinazotumika zaidi ni kunyongwa, sumu ya dawa, kuzama majini, kutumia bunduki, kutumbukia kwenye ulevi au kutumia dawa kupita kiasi.”

Hali hii inafafanuliwa kama sehemu ya njia ndogo za hatua zinazopatikana kutibu na kuzuia mambo ya hatari, ikiwa ni pamoja na matatizo ya akili katika eneo ambalo lina daktari mmoja wa magonjwa ya akili kwa kila wakazi 500,000, ambayo ni mara 100 chini ya mapendekezo ya WHO.

WHO inasema, kampeni ya kuzuia magonjwa hayo inazinduliwa katika maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani, Oktoba 10, ikiendeshwa kwenye mitandao ya kijamii, na inayolenga kufikia watu milioni 10 katika kanda ili kuongeza ufahamu miongoni mwa umma na kuhamasisha uungwaji mkono wa serikali .

Wataalamu wa afya ya msingi, wanapewa mafunzo nchini Zimbabwe kama sehemu ya mpango wa WHO ambapo nchi za Kenya, Uganda, Zimbabwe, Cape Verde na Côte d’Ivoire zikishauriwa kufanya uchambuzi wa kitaifa wa hali ya kujiua wakati uchunguzi ukionesha barani Afrika, kwa kila mtu anayemaliza kujiua, kuna takriban watu 20 waliojaribu kujiua.

Wizara ya Afya yathibitisha uwepo homa ya Nguruwe
Zamalek yakataa kucheza Dar es salaam