Katika kutekeleza mpango wa kulinda mazingira na kuunga mkono juhudi za Serikali za kuifanyaTanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo 2025, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), imesimika mtambo wa kuchenjua kaboni ‘makinikia’ yanayotokanana shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu wenye thamani ya Shilingi bilioni moja.

Hatua hiyo, inaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuwa na mtambo huo ambapo awali kampuni hiyo ilikuwa ikifuata huduma hiyo nchini Afrika Kusini, ambapo Waziri wa Madini, Dotto Biteko alitembelea kampuni hiyo akilenga kujua maendeleo ya GGML baada ya kuanza shughuli za uchimbaji wa chini ya ardhi katika migodi yake mitatu.

Makamu Rais wa AngloGold Ashanti anayeshughulikia Miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo alisema mradi huo utaongeza mapato kwa Serikali na kampuni hiyo na kuongeza kuwa, “Hatuyatupi mabaki yadhahabu na mabaki yenye asili ya hewa ukaayanayoingia kwenye mazingira kwa sababu dunia ipo kwenye mapambano ya kupunguza hewa ya ukaa.”

Awali akizungumzia mradi huo, Dkt. Biteko alisema kaboni zilizokuwa zinazalishwa kwenye migodi iliyopo nchini zilikuwa zinasafirishwa kwenda nje yanchi na kuongeza kuwa, “Tulizuia watu wakadhani tunafanya kitu kibaya, sasa GGML wameweka mtambo kwa ajili kuprocess upya kaboni za dhahabu na kupata dhahabu safi badala ya kusafirishaile kaboni kupeleka nje ya nchi.”

Hatuwezi kuepuka mabadiliko siasa za Ulimwengu: Othman
Mwenge kuzindua miradi ya Mabilioni Kagera