Waziri kiongozi wa Scotland, Nicola Sturgeon amethibitisha kuwa anajiuzulu wadhifa wake aliodumu nao kwa kipindi cha zaidi ya miaka minane.
Kiongozi huyo wa Chama cha Kitaifa cha Scotland, anachukua hatua hiyo huku akiacha maswali juu ya mrithi wa kiti hicho na suala la sintofahamu ya uhuru wa Scotland ambalo bado halijapatiwa ufumbuzi.
Sturgeon alisema atabaki ofisini hadi mrithi wake atakapochaguliwa, na yeye ni Waziri kiongozi aliyekaa muda mrefu zaidi na mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo.
Sturgeon, alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama tawala cha Scottish National-SNP, wakati wa kura ya maoni ya uhuru wa Scotland ya mwaka 2014 na aliapa kuendeleza ushinikizaji wa uhuru wa Taifa hilo na kutetea rekodi yake kuhusiana na suala hilo.